WALIO KATISHA MASOMO KUTOKANA KUPATA UJAUZITO WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWAPA NAFASI YA KUREJA SHULENI KUENDELEA NA MASOMO.
Wanafunzi wa kike waliokatisha masomo yao ya elimu ya sekondari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupata ujazito, wamemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia nafasi ya kurudi shuleni kuendelea na masomo ya Elmu ya sekondari.
Hayo yamejiri 26/09/2023 Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, katika kituo cha Mafunzo Elimj kwa watu wazima mradi wa SEQUIP shule ya Sekonadari Kiwira ambapo Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Maafisa Elimu ya watu wazima na Wenyeviti wa Kamati huduma ya Jamii katika Halmashauri 7 za Mkoa wa Mbeya walifika tembelea kituo cha SEQUIP kiwira katika maadhimisho ya Juma la Elimu ya watu wazima.
Jumla ya wanafunzi wa kike 43 wanaendelea na masomo yao ya sekondari wakiwa ni miongoni wanafunzi waliyo katisha masomo yao hapo awali kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupata ujazito wakiwa masomoni.
Irene Isac Joseph ni miongoni mwa Wanafunzi wanaoendelea na masomo ya sekondari katika kituo cha SEQUIP Kiwira, anaeleza kwamba vishawishi vilimpelekea kushindwa kuendelea na masomo yake ya sekondari baada ya kubeba ujauzito. " Sisi watoto wa kike tuna kabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo vishawishi vya kidunia, usipokuwa makini ni rahisi sana kushawishika, mimi nilibeba ujauzito hali iliyopekea kuacha masomo, ndoto yangu ilikuwa kuja kuwa Daktari lakini niliona siwezi ifikia baada ya kuacha masomo, lakini nina mshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia nafasi hii turudi shuleni kuendelea na masomo, ninaamini ndoto yangu ya kuwa Daktari itamia" alisema Irene.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ambaye ni Diwani wa Kata ya Ipagika, Mh.Mekara O.Mwang'ombola alisema kuwa ni lazima sasa jamii ihamasike kwa ujumla kuwaibua watoto wote waliyokatisha masomo yao hapo awali kutokana na changamoto za ujauzito na sababu zingine waingizwe katika mpango wa SEQUIP na mafunzo ya Elimu ya vitendo kwa watu wazima ili wapate elimu na maarifa yatayowasidia kufikia ndoto zao.
Mkoa wa Mbeya una jumla ya vituo 12 vinayohudumia watoto wa kike waliyo katisha masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo hali duni ya kimaisha, ujauzito, utoro na Ugonjwa.
Kituo cha SEQUIP-AEP Kiwira Sekondari kipo kijiji cha Ilundo, Kata ya Kiwira Wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya kilanza rasmi 18/02/2022 baada ya Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuamua kuwarejesha shuleni Watoto wenye umri kuanzia miaka 13-21 waliyokatiza masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikwemo utoro, ujauzito, ugonjwa na hali duni ya maisha.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.