Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo jana, umekabidhi pikipiki 13 kwa Waratibu wa elimu kata za Busokelo.
Akikabidhi pikipiki hizo zilizotolewa na Serikali kupitia mradi wa LANES ambayo inafadhiliwa na umoja wa mataifa, Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Busokelo, Mhe. Uswege Mbamba, aliwaasa waratibu hao kuwa makaini na matumizi ya vyombo hivyo vya Serikali.
“kuletwa kwa pikipiki hizi katika Halmashauri ya Busokelo itakuwa ni chachu ya kuongeza kiwango cha taaluma na ufaulu wa darasa la nne, saba na kiadato cha 2, 4 na 6”. Alisema Mhe. Mbamba
Mhe. Mbamba aliongeza kuwa ufumbuzi wa vyombo vya usafiri kwa waratibu wa elimu kata ambao ndio wasimamizi wakuu wa elimu ngazi ya kata limepata dawa ya kudumu kwani jiografia ya Busokelo kila mtu anaielewa changamoto yake.
Aidha Mhe. Mbamba alitoa rai kwa waratibu hao kufuata miongozo ya matumizi ya vyombo hivyo vya moto iliyotolewa na Waziri mwenye dhamana ya elimu ili pikipiki hizo ziweze kudumu kwa muda mrefu na matumizi yenye tija.
Akisoma taarifa mbele ya Mgeni rasmi, Afisa Elimu Msingi wa Wilaya Bw. Atuvonwe Chaula alisema kuwa Halmashauri ya Busokelo ni miongoni mwa halmashauri nchini zilizopata pikipiki kwa ajili ya ufuatiliaji wa elimu ngazi ya Kata, ambapo alifafanua kuwa LANES ni kifupisho cha manaeno “Literature And Numerous Education Support” ambapo lengo kuu ni kuimarisha Stadi za Msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu “KKK” kwa rika la kuanzia miaka 5 hadi 13 kwa watoto wasiokuwa na mfumo rasmi na walio katika mfumo rasmi.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.