Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Albert Chalamila amewaasa watumishi wa Halmashauri ya Busokelo kutojihusisha na siasa zinazokinzana na mipango ya Serikali ‘domokrasia’.
Ameyaongea hayo leo mjini Lwangwa wakati wa kikao na watumishi wa halmashauri ikiwa ni ziara yake rasmi ya kujitambulisha kwa watumishi tangu kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mwezi Julai mwaka huu.
“Kwa lugha iliyo nyepesi ni kwamba umechaguliwa kuwa mtumishi wa umma, hiyo ndiyo demokrasia yenyewe, maana kuna kuna watu wanalalamika kuwa Mhe. Rais ameondoa demokrasia… hajaondoa demokrasia bali ameondoa domokrasia kwani domokrasia ni siasa katika utendaji”. Alisema Mhe. Chalamila
Aliongeza kuwa watumishi wa umma wanapaswa kuwa waadilifu na kutii sharia, kanuni na taratibu za utumishi wa umma kama zinavyowataka kuzifuata, kwani ni utovu wa nidhamu kumkuta tumishi wa umma anashinda kwenye vilabu vya pombe akiwa amelewa analaumu na anatoa siri za Serikali.
Aidha alisisitiza ushirikiano miongoni mwa watumishi ili kuleta tija ya utendaji wa kazi na si kuingiliana katika majukumu jambo ambalo linaleta migongano katika maeneo ya kazi na kuleta mifarakano katika utumishin wa umma.
Mhe. Chalamila amekuwa katika ziara rasmi ya kujitambulisha katika Wilaya zake za Mkoa wa Mbeya tangu alipoteuliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mwezi Julai, 2018 akichukua nafasi ya Mhe. Amos Makala ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Katavi.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.