Msimamizi wa Uchaguzi Halmshauri ya Wilaya ya Busokelo Adv.Peter Salama akitoa Elimu ya Umhimu wa kujiandikisha katika Orodha ya Wakazi katika kitongoji cha Itiki kata ya Lwangwa 11/10/2024.
Adv.Salama amefika katika Kijiji cha Kitali Kata ya Lwangwa kwa lengo la kukagua vituo vya Uandikisha ili kuona namna zoezi hilo linavyoendelea na kisha kuwahamasisha Wananchi kuhakikisha Wanajiandikisha katika Orodha ya Mkaazi ili wapate sifa ya Kushiriki Uchaguzi wa serikali za Mitaa ifikapo Novemba 27 2024.
sifa za kujiandikisha katika Orodha ya Wapiga kura katika Daftari la Wakaazi.
1.Uwe Rai wa Tanzania.
2. Uwe na Umri wa miaka 18 na kuendelea
3.Uwe Mkazi wa kitongoji husikia
4.Uwe na akili timamu.
Naye Diwani wa Kata ya Lwangwa Mhe.Jackosnj Mwampulule ambaye ni Mkazi wa Kitongoji cha Itiki amehimizia wananchi Wote kuhakikisha wanajiandikisha katika Orodha ya Wapiga kura kwa muda wa siku kumi zilizopangwa kuanzia leo 11/10/ 2024. hadi 21/10/2024.
"Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.